Add parallel Print Page Options

Mwishie Mungu

11 Rafiki zangu, ninawasihi kama wapitaji na wageni katika ulimwengu huu kuwa mbali na tamaa za kimwili, ambazo hupingana na roho zenu. 12 Muwe na uhakika wa kuwa na mwenendo mzuri mbele ya wapagani, ili hata kama wakiwalaumu kama wakosaji, watayaona matendo yenu mazuri nao wanaweza kumpa Mungu utukufu katika Siku ya kuja kwake.

Tii Mamlaka Yote ya Kibinadamu

13 Nyenyekeeni kwa mamlaka yo yote ya kibinadamu kwa ajili ya Bwana. Mnyenyekeeni mfalme, aliye mamlaka ya juu kabisa.

Read full chapter