Ninyi pia, kama mawe hai mjengwe kuwa nyumba ya kiroho, mpate kuwa makuhani watakatifu, mkitoa sadaka za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, ninaweka jiwe kuu la msingi huko Sayuni; jiwe la pembeni teule na la thamani kubwa, na kila amwaminiye hataaibika.” Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani kubwa. Lakini kwao wasioamini, “Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi,”

Read full chapter