10 Maana kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote. Tamaa ya fedha imewafanya wengine watangetange mbali na imani na kuteseka kwa huzuni nyingi.

Mawaidha Ya Paulo Kwa Timotheo

11 Lakini wewe mtu wa Mungu, epuka haya yote. Tafuta kupata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole. 12 Pigana ile vita njema ya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa ulipokiri lile ungamo lako jema mbele ya mashahidi wengi.

Read full chapter