Mawaidha Ya Paulo Kwa Timotheo

11 Lakini wewe mtu wa Mungu, epuka haya yote. Tafuta kupata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole. 12 Pigana ile vita njema ya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa ulipokiri lile ungamo lako jema mbele ya mashahidi wengi.

13 Mbele ya Mungu ambaye amevipa vitu vyote uhai, na mbele ya Kristo Yesu ambaye kwa ushuhuda wake mbele ya Pontio Pilato alikiri lile ungamo jema,

Read full chapter