18 Waambie watende wema, wawe matajiri katika matendo mema, wawe wakarimu na tayari kushiriki mali zao na wengine. 19 Kwa njia hii watajiwekea msingi imara kwa wakati ujao na hivyo watajipatia uzima ambao ni uzima kweli.

20 Timotheo, tunza vema yote uliyokabidhiwa. Epuka majadil iano yasiyo ya Mungu na mabishano ambayo kwa makosa huitwa elimu.

Read full chapter