Add parallel Print Page Options

Baadhi ya watumwa wanao mabwana ambao ni waamini, hivyo hao ni ndugu. Je, inamaanisha wasiwaheshimu mabwana zao? Hapana, watawatumikia hata kwa uzuri zaidi, kwa sababu wanawasaidia waaminio, watu wawapende.

Haya ni mambo ambayo lazima uyafundishe na kumwambia kila mtu kufanya.

Mafundisho ya Uongo na Utajiri wa Kweli

Watu wengine wanafundisha uongo na hawakubaliani na mafundisho ya kweli ambayo yanatoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Hawakubali mafundisho ambayo yanatuongoza kumheshimu na kumpendeza Mungu. Wanajivunia wanayoyafahamu, lakini hawaelewi chochote. Wamepagawa na wana ugonjwa wa kupenda mabishano na mapigano ya maneno. Na hayo yanaleta wivu, ugomvi, matusi, na uovu wa kutoaminiana.

Read full chapter