Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. Kama nikitoa mali yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.

Read full chapter