16 wanajaribu kutuzuia tusiwahubirie watu wa mataifa mengine ujumbe ambao utawaokoa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia.

Paulo Atamani Kuwaona Wathesalonike

17 Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa muda, ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu si kwa moyo, tulizidi kwa hamu kubwa kufanya kila jitihada tuonane uso kwa uso. 18 Maana tulitaka kuja huko, hasa mimi Paulo, nilijaribu zaidi ya mara moja, lakini shetani akatuzuia.

Read full chapter