12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu.

Read full chapter