Add parallel Print Page Options

17 Kama pendo la Mungu limekamilishwa ndani yetu, tunaweza kuwa bila hofu siku ambayo Mungu atahukumu ulimwengu. Hatutakuwa na hofu, kwa sababu katika ulimwengu huu tunaishi kama Yesu.[a] 18 Palipo na upendo wa Mungu, hakuna hofu, kwa sababu upendo wa Mungu ulio kamili unaondoa hofu. Ni hukumu yake ndiyo inayomfanya mtu kuwa na hofu. Hivyo pendo lake halikamilishwi kwa mtu ambaye ndani yake kuna hofu.

19 Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda sisi kwanza.

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:17 Yesu Kwa maana ya kawaida, “Yeye Yule”.