12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.

Uzima Wa Milele

13 Ninawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu kusudi mjue kuwa mnao uzima wa milele. 14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia.

Read full chapter