Font Size
1 Yohana 5:16-18
Neno: Bibilia Takatifu
1 Yohana 5:16-18
Neno: Bibilia Takatifu
Umuhimu Wa Kuonyana
16 Mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyompeleka kwe nye kifo, amwombee kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Ninasema kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi ambayo humpeleka mtu kwenye kifo. Sisemi kwamba ana paswa kuomba kuhusu hiyo. 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi na kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.
18 Tunafahamu kuwa kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda na yule mwovu hawezi kumgusa.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica