Add parallel Print Page Options

Na sasa, mwanamke mwema, nina ombi hili: na tupendane sisi kwa sisi. Hii si amri mpya. Ni amri ile ile tuliyo kuwa nayo tangu mwanzo. Na hii ndiyo maana ya kupenda: kuishi kulingana na amri zake. Na amri ya Mungu ni hii: Kwamba muishi maisha ya upendo. Mliisikia amri hii toka mwanzo.

Walimu wengi wa uongo wamo duniani sasa. Wana kataa kusema Yesu ni Masihi aliyekuja duniani na kufanyika mwanadamu. Kila anayekataa kuikubali kweli hii ni mwalimu wa uongo na adui wa Kristo.

Read full chapter