10 Kwa hiyo nitakapokuja nitaeleza mambo anayofanya; na kuhusu maneno maovu anayosema juu yangu. Wala hatosheki na hayo bali anakataa kuwakaribisha ndugu. Pia anawazuia wale ambao wanataka kuwakarib isha na anawafukuza kutoka katika kanisa. 11 Mpendwa, usiige ubaya bali iga wema. Atendaye mema ni wa Mungu. Atendaye uovu hajapata kumwona Mungu. 12 Demetrio anashuhudiwa wema na kila mtu na hata kweli yenyewe inamshuhudia. Mimi pia ninamshuhudia wema, na wewe unajua kwamba ushuhuda wangu ni wa kweli.

Read full chapter