Diotrefe Na Demetrio

Niliandika barua kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe apendaye kujiweka mbele kama kiongozi wao, hatambui mamlaka yangu. 10 Kwa hiyo nitakapokuja nitaeleza mambo anayofanya; na kuhusu maneno maovu anayosema juu yangu. Wala hatosheki na hayo bali anakataa kuwakaribisha ndugu. Pia anawazuia wale ambao wanataka kuwakarib isha na anawafukuza kutoka katika kanisa. 11 Mpendwa, usiige ubaya bali iga wema. Atendaye mema ni wa Mungu. Atendaye uovu hajapata kumwona Mungu.

Read full chapter