Wagalatia 3:21-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Lengo la Sheria ya Musa
21 Je, hili lamaanisha kwamba sheria hutenda kazi kinyume na ahadi za Mungu? La hasha. Sheria iliyotolewa kamwe haikuwa na uwezo wa kuwaletea watu maisha mapya. Ingekuwa hivyo, basi tungehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kuifuata sheria. 22 Lakini hilo halikuwa kusudi la sheria. Maandiko yanauweka ulimwengu wote chini ya udhibiti wa dhambi kama aina ya kifungo gerezani. Ili kile ambacho Mungu aliahidi kipokelewe kwa njia ya imani katika[a] Yesu Kristo. Hii hutolewa kwa wale wanaomwamini.
23 Kabla ya aliye mwaminifu kuja, sheria ilituweka sisi kama wafungwa. Hatukuwa huru hadi imani hii inayokuja[b] ilipofunuliwa kwetu. 24 Nina maana kuwa sheria ilikuwa ni mlezi aliyetusimamia[c] tu hadi Kristo alipokuja. Baada ya kuja kwake, tungefanyika kuwa wenye haki mbele za Mungu kwa njia ya imani. 25 Sasa kwa sababu imani hii imekuja, hatuhitaji tena kusimamiwa na kulelewa na sheria.
Read full chapterFootnotes
- 3:22 imani katika Au “uaminifu wake”.
- 3:23 imani hii inayokuja Au “imani ya Yesu”.
- 3:24 mlezi aliyetusimamia Ina maana kama ile ya mlezi wa watoto yaani yaya; Kwa Kiyunani namaanisha mtu, kwa kawaida aliyekuwa mtumwa, aliyemsindikiza mvulana mdogo kwenda shule toka nyumbani na kuhakikisha ya kwamba mvulana yule anaenenda vizuri na hapati matatizo.
© 2017 Bible League International