Add parallel Print Page Options

Watu Wanaobarikiwa na Mungu

27 Yesu alipokuwa akisema mambo haya, mwanamke mmoja katika kundi la watu akapaza sauti akamwambia “Amebarikiwa na Mungu mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!”

28 Lakini Yesu akasema, “Wamebarikiwa zaidi wanaosikia na kuyatii mafundisho ya Mungu.”

Baadhi ya Watu Wawa na Mashaka na Mamlaka ya Yesu

(Mt 12:38-42; Mk 8:12)

29 Baada ya kundi la watu kuongezeka na kumzunguka, Yesu alisema, “Ninyi watu mnaoishi sasa ni waovu. Mnaomba muujiza kama ishara kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna muujiza utakaofanyika ili kuwathibitishia jambo lolote. Ishara pekee mtakayopata ni kile kilichompata Yona.[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 11:29 Yona Nabii katika Agano la Kale. Baada ya siku tatu akiwa katika tumbo la samaki, alitoka akiwa hai. Kisha alikwenda katika mji uliojaa uovu, mji wa Ninawi ili kuwapa watu maonyo ya Mungu.