Add parallel Print Page Options

32 Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa mtafananishwa pia na watu wa Ninawi, nao watakuwa mashahidi watakaoonyesha makosa yenu. Ninasema hivi kwa sababu Yona alipowahubiri, walibadili mioyo na maisha yao. Na sasa mnamsikia mtu aliye mkuu kuliko Yona, Lakini hamtaki kubadilika!

Iweni Mwanga kwa Ajili ya Ulimwengu

(Mt 5:15; 6:22-23)

33 Hakuna mtu anayechukua taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunika. Badala yake huiweka mahali palipo wazi, ili wanaoingia ndani waweze kuiona nuru yake. 34 Namna unavyowatazama watu inaonesha kwa hakika jinsi ulivyo. Unapowatazama watu katika hali isiyo ya ubinafsi, inaonesha wazi kuwa umejaa nuru. Lakini unapowatazama watu katika namna ya uchoyo, ni wazi kuwa umejaa giza.[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 11:34 Kwa maana ya kawaida, “Taa ya mwili ni jicho lako. Unapowatazama watu bila kuwa na kinyongo, mwili wako wote unakuwa umejaa nuru. Lakini ikiwa jicho lako ni la uovu, mwili wako una giza.”