22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo ninawaambia, msihangaikie maisha yenu, kwamba mtakula nini; au miili yenu kwamba mtavaa nini. 23 Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege!

Read full chapter