23 Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege! 25 Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja?

Read full chapter