11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”

Read full chapter