Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’

“Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko watu wa nuru kukamilisha mambo yao. Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.

Read full chapter