Add parallel Print Page Options

Kuja Kwa Ufalme Wa Mungu

(Mt 24:23-28,37-41)

20 Baadhi ya Mafarisayo walimuuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu utakuja lini?” Yesu akajibu, “Kuja kwa ufalme wa Mungu si kitu unachoweza kuona. 21 Watu hawatasema, ‘Tazama ufalme wa Mungu uko hapa’ au ‘Ule pale!’ Hapana, Ufalme wa Mungu upo hapa pamoja nanyi.”[a]

22 Kisha Yesu akawaambia wafuasi wake, “Wakati utakuja, ambapo mtatamani angalau kuwa na Mwana wa Adamu hata kwa siku moja, lakini hamtaweza.

Read full chapter

Footnotes

  1. 17:21 Mungu upo hapa pamoja nanyi Au “umo ndani yenu”.