Add parallel Print Page Options

35 Hivyo wafuasi wakampeleka punda kwa Yesu. Wakatandika baadhi ya nguo zao juu ya mwanapunda, kisha wakampandisha Yesu juu yake. 36 Yesu akaanza kwenda Yerusalemu. Wafuasi walikuwa wanatandaza nguo zao njiani mbele yake.

37 Yesu alipokaribia Yerusalemu. Alipokuwa katika njia inayotelemka kutoka kwenye Mlima wa Mizeituni, kundi lote la wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa kupaza sauti. Walimsifu Mungu kwa furaha kwa sababu ya miujiza yote waliyoiona.

Read full chapter