Add parallel Print Page Options

36 Yesu akaanza kwenda Yerusalemu. Wafuasi walikuwa wanatandaza nguo zao njiani mbele yake.

37 Yesu alipokaribia Yerusalemu. Alipokuwa katika njia inayotelemka kutoka kwenye Mlima wa Mizeituni, kundi lote la wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa kupaza sauti. Walimsifu Mungu kwa furaha kwa sababu ya miujiza yote waliyoiona. 38 Walisema,

“Karibu! Mungu ambariki mfalme
    ajaye kwa jina la Bwana!(A)
Amani iwe mbinguni,
    na utukufu kwa Mungu!”

Read full chapter