Add parallel Print Page Options

44 Watakuteketeza wewe na watu wako wote. Hakuna jiwe hata moja katika majengo yako litaachwa juu ya jiwe jingine. Haya yote yatatokea kwa sababu hukujua wakati ambao Mungu alikuja kukuokoa.”

Yesu Asafisha Eneo la Hekalu

(Mt 21:12-17; Mk 11:15-19; Yh 2:13-22)

45 Yesu aliingia katika eneo la Hekalu. Akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wanauza vitu humo. 46 Akasema, “Maandiko yanasema, ‘Hekalu langu litakuwa nyumba ya sala.’(A) Lakini mmeligeuza kuwa ‘maficho ya wezi.’”(B)

Read full chapter