45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni. 46 Akawauliza, “Mbona mnalala? Amkeni muombe ili msiingie katika majaribu.”

Yesu Akamatwa

47 Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, pakatokea kundi la watu likiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wana funzi kumi na wawili. Akamsogelea Yesu ili ambusu.

Read full chapter