55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57 Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!”

Read full chapter