10 Naye akawajibu, “Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano ili, ‘Kuangalia waan galie lakini wasione, kusikia wasikie, lakini wasielewe.’ 11 Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. 12 Ile njia zilipoanguka baadhi ya mbegu, ni mfano wa watu wanaolisikia neno la Mungu lakini shetani huja akalichukua kutoka katika mioyo yao, ili wasiamini na kuokolewa.

Read full chapter