11 Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. 12 Ile njia zilipoanguka baadhi ya mbegu, ni mfano wa watu wanaolisikia neno la Mungu lakini shetani huja akalichukua kutoka katika mioyo yao, ili wasiamini na kuokolewa. 13 Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao.

Read full chapter