13 Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao. 14 Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua. 15 Bali ule udongo mzuri ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mwema na wa utii, wakavumilia na kuzaa matunda.”

Read full chapter