18 Kwa hiyo muwe waangalifu mnaposikiliza, kwa sababu, yeye aliye na kitu ataonge zewa, naye ambaye hana, atanyang’anywa hata kile anachodhania anacho.”

Ndugu Wa Kweli

19 Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kum wona lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. 20 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.”

Read full chapter