Add parallel Print Page Options

Zilizosalia ziliangukia kwenye udongo mzuri wenye rutuba. Mbegu hizi zikaota na kuzaa kila moja mia.”

Yesu akamalizia fumbo. Kisha akapaza sauti, akasema, “Ninyi watu mnaonisikia, sikilizeni!”

Wafuasi wake wakamwuliza, “Fumbo hili linamaanisha nini?”

10 Akasema, “Mmechaguliwa kujua kweli za siri kuhusu ufalme wa Mungu. Lakini ninatumia mafumbo kuzungungumza na watu wengine. Ninafanya hivi ili,

‘Watazame,
    lakini wasiweze kuona.
Wasikia,
    lakini wasielewe.’(A)

Read full chapter