Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

32 “Hakuna ajuaye siku hiyo itakuwa lini au saa ngapi; hata malaika mbinguni hawajui wala mimi Mwana sijui, isipokuwa Mungu Baba peke yake. 33 “Jiandaeni, muwe macho. Kwa maana hamjui wakati mambo haya yatakapotokea. 34 Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.

Read full chapter