Font Size
Marko 14:1-3
Neno: Bibilia Takatifu
Marko 14:1-3
Neno: Bibilia Takatifu
Mpango Wa Kumwua Yesu
14 Siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na sherehe ya mikate isiyotiwa chachu, makuhani wakuu na walimu wa sheria wali kuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa siri na kumwua. 2 Wakaambiana, “Jambo hili tusilifanye wakati wa sikukuu maana watu wanaweza kufanya ghasia.”
Yesu Apakwa Manukato
3 Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni ambaye aliwahi kuwa na ukoma. Alipokuwa mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia ndani akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu manukato hayo kichwani.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica