Yesu Apakwa Manukato

Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni ambaye aliwahi kuwa na ukoma. Alipokuwa mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia ndani akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu manukato hayo kichwani. Baadhi ya watu waliokuwapo wali chukia wakasema, “Kwa nini anapoteza bure manukato hayo? Si afadhali yangeliuzwa kwa dinari zaidi ya mia tatu na fedha hizo wakapewa maskini?” Wakamkemea huyo mama kwa hasira.

Read full chapter