31 Tunaweza kuufa nanisha na punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. 32 Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wakaweza kujenga viota kwenye kiv uli chake.”

33 Yesu alitumia mifano mingine mingi kama hii kuwaelezea neno la Mungu, kwa kadiri walivyoweza kuelewa.

Read full chapter