32 Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wakaweza kujenga viota kwenye kiv uli chake.”

33 Yesu alitumia mifano mingine mingi kama hii kuwaelezea neno la Mungu, kwa kadiri walivyoweza kuelewa. 34 Hakuwafundisha lo lote kuhusu Ufalme wa Mungu pasipo kutumia mifano. Lakini ali pokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.

Read full chapter