15 Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”

16 Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema,“Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.”

17 Yesu alifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mna zungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho?

Read full chapter