Akawaambia watu wakae chini. Kisha akaichukua ile mikate saba na baada ya kushukuru akaimega, akawapa wanafunzi wake wawa gawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. Watu walikula wakatosheka na baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba.

Read full chapter