40 Kwa maana ye yote ambaye si adui yetu yuko upande wetu. 41 Ninawahakikishia kwamba mtu atakayewapa japo maji ya kunywa kwa kuwa ninyi ni wafuasi wangu, atapewa tuzo.”

Kuhusu Kuwakwaza Wengine

42 “Na mtu atakayesababisha mmojawapo wa hawa wadogo waniaminio kupoteza imani yake, ingalikuwa nafuu kama mtu huyo angefungiwa jiwe kubwa shingoni akatupwa ziwani.

Read full chapter