Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo

18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Mar ia akiwa bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri. 20 Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi, usisite kumwoa Maria mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Read full chapter