23 Watu wote wakashangaa wakaulizana, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24 Lakini Mafarisayo waliposikia haya wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mfalme wa pepo wote.”

25 Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu.

Read full chapter