24 Lakini Mafarisayo waliposikia haya wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mfalme wa pepo wote.”

25 Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu. 26 Na kama shetani anamfukuza shetani, atakuwa amega wanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utaendeleaje?

Read full chapter