Ishara Ya Yona

38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi.

Read full chapter