40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki; kwa kuwa yeye alisafiri kutoka miisho ya dunia ili akaisikilize hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”

Read full chapter