11 Yesu akajibu, “Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya isipokuwa wale ambao Mungu amewajalia. 12 Kwa maana wako watu wasioweza kuoa kwa sababu wamezaliwa na hali hiyo; na wengine wamefanywa hali hiyo na binadamu; na pia wako wengine ambao wameamua kutokuoa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kuli pokea fundisho hili na alipokee.”

Yesu Awabariki Watoto Wadogo

13 Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Yesu ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wali owaleta.

Read full chapter