73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesi mama pale walimwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao kwa maana namna yako ya kusema ni kama yao.” 74 Ndipo Petro akalaani na kuapa, akawaambia, “Simfahamu mtu huyo!” Wakati huo huo jogoo akawika. 75 Na Petro akakumbuka Yesu alivyomwambia, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.” Akaenda nje, akalia kwa uchungu.

Read full chapter