11 “Mimi nawabatiza kwa maji kama ishara kwamba mmetubu dhambi zenu. Lakini baada yangu anakuja aliye mkuu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuchukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Pepeto lake liko mkononi, naye atasafisha pa kupepetea nafaka, na ngano yake ataiweka ghalani; lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”

Yesu Abatizwa

13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yordani ili abatizwe na Yohana.

Read full chapter