14 Yohana alitaka kumzuia akimwambia, “Mimi ndiye ninahitaji kubatizwa na wewe, mbona unakuja kwangu? ” 15 Lakini Yesu akamjibu, “Kubali iwe hivi kwa sasa; kwa maana inatupasa kutimiza haki yote.” Kwa hiyo Yohana akakubali.

16 Na Yesu alipokwisha kubatizwa alitoka kwenye maji, ghafla mbingu zilifunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua aka kaa juu yake.

Read full chapter